Ukurasa wa nyumbani
 Changia mawazo




Tafsiri:

'العربية / Al-ʿarabīyah
Bahasa Indonesia
Català
中文 / Zhōngwén
Deutsch
English
Español
Filipino/Tagalog
Français
Ελληνικά / Elliniká
हिन्दी / Hindī
Italiano
日本語 / Nihongo
Kiswahili
한국어 / Hangugeo
بهاس ملايو / Bahasa Melayu
Português
Română
Русский
Српски / Srpski
తెలుగు /Telugu
Tiếng Việt

                                        

Kurasa nyingine:

Visomo

Ramani ya tovuti

Maneno muhimu

Wasiliana nasi

Nyaraka za matumizi

Tovuti zinazohusiana

Yaliyomo:

Yaliyomo:

KUCHANGIA MAWAZO;
TARATIBU NA MTINDO

na Phil Bartle, PhD

imetafsiriwa na Lillian Naka


Utaratibu wa mbinu

Mbinu katika matayarisho ya uwezeshaji wa jamii

Mwongozo huu utakuwezesha kukisaidia kikundi kufanya uamuzi kwa pamoja.Mbinu hii yaweza kutumika kwenye mkutano wa kijamii,mkutano wa viongozi wa shirika la kijamii,viongozi wa mashirika yasiyo ya kiserikali,shirika la kiserikali au shirika la umoja wa mataifa, kati ya washiriki watano hadi mia mbili.

Maadamu una ujuzi wa kukiongoza kikao na utahakikisha mtindo na kanuni za kikao zimefuatwa (kwa mfano, hakuna kukosoa au kumsuta mwengine), utakuwa unahakikisha kuwa maamuzi ni ya kundi zima na wala hayakulazimishwa na uwepo wako.Utakuwa una sahilisha uamuzi wa kundi.

Madhumuni ya kikao cha kuchangia mawazo:

Madhumuni ya kikao cha kuchangia mawazo ni kutambua shida na kutafuta kwa pamoja, uamuzi mwafaka wa kutatua shida hiyo.

Mahitaji;

  1. Shida inayohitaji kutatuliwa;
  2. Kikundi chenye uwezo wa kufanya kazi kwa pamoja.Hii hutumika kwa kundi la watu wapatao watano hadi kumi (kwa mfano wafunzi,shirika la wafanyikazi,wanaofanya kazi nje ya ofisi zao), hadi mkutano wamamia ya wanakijiji;
  3. Ubao,kurasa za karatasi kubwa au kitu ambacho kitaonekana vyema na wote, na kalamu zenye maandishi manene;na
  4. Msahalishi(wewe).Mtu ambaye jukumu lake ni kuandika vidokezo vya washiriki wala si maoni yake,na utumie ujuzi wa uongozaji kudhibiti nidhamu na malengo ya kikao.

Kanuni za kimsingi:

  • Msahalishi ataongoza kila kikao;
  • Msahalishi ataalika washiriki kutoa vidokezo;
  • Hakuna kukosoa (dokezo la mwengine);na
  • Vidokezo vyote viandikwe ubaoni (hata vile visivyostahili)

Taratibu:

  1. Fasili au tambua shida:
    • Uliza vidokezo juu ya shida muhimu;
    • Hakuna kukosoa dokezo la mwengine;
    • Andika shida zote zilizodokezwa ,ubaoni
    • Ziweke pamoja, shida zinazoambatana au kuhusiana;kisha
    • Ziandike upya kulingana na umuhimu (zenye umuhimu mkubwa ziwe juu).
  2. Zalisha Lengo:
    • Pindua fasili ya shida (suluhisho lake)
    • Suluhisho la shida iliyofasiliwa hapo juu, ndilo lengo
    • Fasili lengo kama suluhisho la shida;
    • Andika lengo hilo ubaoni; kisha
    • Likumbushe kundi kwamba lengo hilo ndilo walilo chagua
  3. Fasili Nia au shabaha:
    • Elezea tofauti kati ya shabaha au Nia na Lengo;
      Msahalishi anastahili kufahamu haya:(Tazama HODARI;Shabaha, yaweza kukadiriwa,ina kiwango na tarehe ya kumalizika).
    • Uliza kundi litoe vidokezo kuhusu shabaha;
    • Andika vidokezo vyote kuhusu shabaha, Ubaoni;
    • Hakuna anayepaswa kukosoa (kidokezo cha mtu yeyote);
    • Viweke pamoja, vidokezo vinavyohusiana au kuambatana;
    • Viandike upya kulingana na umuhimu wake (vyenye umuhimu mkubwa viwe juu);kisha
    • Wakumbushe washiriki wa kundi kuwa, ni wao, waliozalisha shabaha hizo.
  4. Tambua rasilimali na vizuizi:
    • Uliza kundi litoe vidokezo kuhusiana na rasilimali na vizuizi;
    • Viandike vidokezo vyote kuhusiana na rasilimali na vizuizi, ubaoni;
    • Hakuna anayepaswa kukosoa (kidokezo cha mshiriki yeyote);
    • Ziweke pamoja rasilimali zinazofanana au kuhusiana.
    • Ziandike upya kulingana na kipaumbele (zenye umuhimu mkubwa ziwe juu).
    • Likumbushe kundi kuwa, ni wao waliozalisha orodha hiyo;
    • Viweke pamoja , vizuizi vyote vinavyofanana au vinavyoambatana.
    • Viandike upya kulingana na kipaumbele(vyenye umuhimu mkubwa viwe juu);kisha
    • Likumbushe kundi kuwa, ni wao waliozalisha orodha hiyo.
  5. Tambua mbinu:
    • Uliza kundi litoe vidokezo kuhusu mbinu zitakazotumika;
    • Viandike vidokezo vyote ubaoni;
    • Hakuna apaswaye kukosoa (kidokezo cha mwengine)
    • Viandike pamoja, vidokezo vinavyoambatana au vinavyohusiana ;
    • Viandike upya kulingana na kipaumbele (vyenye umuhimu mkubwa viwe juu);
    • Likumbushe kundi kuwa, ni wao waliozalisha orodha hiyo;
    • Chagua mtindo ulio juu ya orodha.
  6. Andika ubaoni, maamuzi ya kundi kwa ufupi:
    • shida;
    • lengo;
    • shabaha au Nia;
    • rasilimali
    • vizuizi; na
    • mtindo;
    Elezea kundi kwamba, wametengeza mpangilio wa vitendo vitakavyotumika. Ikiwa mtu ataandka yaliyoamuliwa katika kila kitengo kilichotajwa hapo juu,atapata kiini cha waraka wa mpangilio.Waeleze kwamba,wametayarisha mpango huo kwa pamoja na "wanaumiliki".

Mwisho:

Ni nyepesi.Hii haimaanishi kuwa ni rahisi lakini huboreka ikiwa desturi.kwenye kila sehemu ya kikao hicho,waweza tumia michezo ya kuigiza,michezo inayojumuisha kundi na mbinu zengine.Jaribu mitindo tofauti mara kwa mara.

Heri njema na mafanikio kwenye uchochezi wa jamii!

––»«––

Maamuzi kwenye mfano huu yametokana na maswali yale manne ya msingi kuhusu usimamizi.Majibu ya maswahili hayo, ,kwa pamoja, ndio kiini cha ushauri wa mradi.Kama njia mbadala,kikao cha SWOT chawezatumika kwa kundi kubwa.


Kikao cha kuchangia mawazo:


Kikao cha kuchangia mawazo

© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
Web Design: Lourdes Sada
––»«––
Imeratibishwa mwisho: 08.11.2011

 Ukurasa wa nyumbani

 Changia mawazo