Ukurasa wa Nyumbani
Kujitayarisha
Tafsiri:

'العربية / Al-ʿarabīyah
Bahasa Indonesia
Català
Deutsch
English
Español
Français
Ελληνικά / Elliniká
Kiswahili
Српски / Srpski
Türkçe

                                        

Kurasa zengine:

Moduli

Ramani ya Tovuti

Maneno muhimu

Wasiliana nasi

Nyaraka za Matumizi

Viungo muhimu

Hadithi ya Nne

Hakufahamu ujuzi uliohitajika

na Phil Bartle, PhD

imetafsiriwa na Lillian Naka

Vignette

Hadithi fupi zinazoelezea kanuni

Shamim alikuwa na talanta asili ya uigizaji. Alikuwa na uwezo wa kuchukua majukumu tofauti kama ilivyohitajika. Alipoanza kuiandaa Jamii, alihisi kama Jamii haikumakinika kwa mambo muhimu kama; haja ya kuwa na maji safi, mafunzo kuhusu usafi, njia bora za utupaji taka. Labda dhana yake haikuwa sawa.

Lakini alichokosa kufahamu ni kwamba, iwapo atajidai mjuaji, na kuiona Jamii kama isiyo na ufahamu wa mambo, Jamii itahisi kutengwa na kupoteza hamu ya kutaka kujumuishwa.

Mwanzoni, alitenda kosa hilo la kuwa mjuaji na kuiona Jamii kama isiyofahamu mambo, kwa bahati nzuri, mwenzake alimtahadharisha na kumwarifu atumie njia ya usawa. Kwa bahati nzuri, alikuwa na uwezo wa kutumia talanta yake asilia hivyo basi alihitaji tu kuelezwa alichohitaji kufanya ili apate matokeo bora. Alibadili mbinu kwa haraka na kufaulu kuihamasisha jamii kuboresha afya yao kwa kuzuia maradhi yanayo sambazwa kwa maji.

Kumbuka:
Hadithi hizi zimetokana na matukio ya kweli. Majina ya watu na mahali yamebadilishwa ili kuficha uhalisia.

──»«──
Ukinakili kutoka kwa tovuti hii, tafadhali mkiri mwandishi/ Waandishi
na uihusishe kwa www.cec.vcn.bc.ca/cmp/indexks.htm

© Hati miliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
Mtandao umebuniwa na Lourdes Sada
──»«──
Imeratibishwa mwisho: 2013.12.04

 Ukurasa wa nyumbani
Kujitayarisha