Ukurasa wa nyumbani
 Janga
Tafsiri:

Català
中文 / Zhōngwén
Deutsch
English
Español
Filipino/Tagalog
Français
Ελληνικά / Elliniká
Italiano
Kiswahili
Polszczyzna
Português
Română
Српски / Srpski

                                        

Kurasa zengine:

Visomo

Ramani ya tovuti

Maneno muhimu

Wasiliana nasi

Nyaraka za matumizi

Tovuti zinazohusiana

Kurasa nyingine:

Kurasa nyingine:

Kurasa nyingine:

Kurasa nyingine:


SWOT KWA AJILI YA MABADILIKO

na Phil Bartle, PhD

imetafsiriwa na Jacob Lisakafu


Reference

Uimara,udhaifu,fursa,na vikwazo, kuchangia kutoka kwa wadau,wafanyakazi, wanaojitolea, na wanachama wa Jumuia ambao ni muhimu kwa kuandaa malengo ta taasisi na mipango yao, na kuangalia mambo muhimu ya kuleta mabadiliko.

Utangulizi:

Mikutano ya SWOT maana yake ni kupata orodha ya mambo yatakayotokea na uwelekea wake na umuhimu wake kwa kupanga mipango.Inaweza kutumika katika mikutano mikubwa ambayo washiriki watakuja kutoka sehemu mbali mbali na taasisi zao.SWOT inaweza kutumika katika jamuia au jamii kwa kuwa katibu na taasisi pale ambapo washiriki awalipwi na wanachama ni wakazi wa hapo.Inaweza kutumika katika taasisi, kama NGO,Idara za serikali au kampuni binafsi na pale wanachama wanakuwa ni wa kujitolea na bila kulipwa.

Nakala hii ya kufundishia, inaelezea kipindi cha SWOT. Inaweza kutumiwa na Taasisi saidizi (NGO,Miradi ya maendeleo, au taasisi ya serikali) ambazo zinaangalia namna ya kubadilisha program kutoka kuwa program ya kutoa misaada katika kwenda kwenye program ya kusaidia kwenye maendeleo,na kusimamia kwenye njia ya uwezeshaji. Angalia: Kutoka kutoa misaada kuelekea uwezeshaji.

SWOT inaweza kutumiwa katika kubadilisha program, na inapendekezwa kutumiwa katika kipindi cha kila mwaka au kila kipindi cha kupitia.

SWOT ni kifupi cha maneno manne inasimama kwa: Uimara (Strenghts),udhaifu (Weaknesses),fursa (Opportunities),vikwazo (Threats).

Maelezo kwa Vitendo:

Uimara wa nini? Udhaifu wa nini?

Mtu mmoja mmoja (wafanyakazi,watu wa kujitolea, wadau, wakazi),kupanga muundo (muundo na taratibu),program au mpango wa kazi,uongozi,mtiririko wa material, mtiririko wa habari, kufanya maamuzi, mazingira (jamii, physical, siasa, biological, sheria, utawala, uchumi);zote hizi ni uimara na udhaifu, Ni nini hizi?

Fursa ya nini? vikwazo vya nini?

Wapi na inabidi taasisi, program na watu wanaenda kutokea hapa?nini wanachangia kufika pale? wapi wanasimama.

Malengo ni muhimu,kabla ya mipango yoyote haijafanyika. kama ni hali halisi na kweli inatekeleza,inaweza isifanikiwe. Inategemea huwakiki wa kuona na hali halisi itakayochangia katika mafanikio.

Nini chanzo kizuri kulinganisha na vikundi shirikishi vya kuwashirikisha wadau, wwafanyakazi,watu wa kujitolea, na Jumuia?

A Njia shirikishi:

Kipindi cha SWOT ni njia ya kupata habari kutoka kwa washiriki. Habari hizo zinahusu kuangalia hali halisi na kufanya analysis ya hali halisi zinazoonwa na washiriki.Kipindi cha chemshabongo ni kwa mwendeshaji kujaribu kupata uchangiaji wa washiriki na wanachama wote, hasa kwa mtu mmoja mmoja ambao hawazungumzi mara kwa mara.

kwa kufanya hivyo,inatazamiwa kuchangia mawazo ya watu waliochangia katika mikutano au kipindi cha SWOT, kuandika ukweli halisi na sio kushusha umuhimu wa issues.

Kipindi hiki ni kizuri kufanywa kama washiriki wote wana elimu na wanaweza kuandika wenyewe mawazo wanachochangia. Kama washiriki hawana elimu ya kutosha, mkutano unaweza kufanyiwa mabailiko na watoto wanaweza kuja pamoja na wazazi wao hili kuwasaidia kuandika maoni yao.

Katika mkutano (na washiriki wote), muongozaji mkutano aandike maneno manne katika ubao:Uimara,Udhaifu,Fursa,and Vikwazo.Mazungumzo ya kawaida yafuatie.Kama wakala atapenda kuibadilisha program yenyewe kutoka program ya kusaidia kwenye janga kuwa program ya uwezeshaji na kutoa misaada ya maendeleo, kuangalia zaidi program ya uwezeshaji. Mwongozaji wa mkutano aonyeshe baadhi ya tabia ya taasisi, na kuwaomba washiriki kuangalia katika Uimara na udhaifu ambao utachangia katika kukua au kuzuia maendeleo ya kukua kwa taasisi.

Kama kikundi kipo kwenye mkutano wa mwaka au nusu mwaka wa kupitia program, malengo na matazamio ya hiyo taasisi lazima yafahamike.lakini yanaweza kuandikwa kwa kifupi katika kipindi hicho. Msimamiaji lazima aakikishe aina ya information zinazoitajika zinaeleweka na washiriki wote kwa washirii kuzitaja kwenye mkutano kwa mdomo. Msimamiaji awaulize washiriki kuandika wachangiaji kuandika katika karatasi,kila moja katika karatasi yake bila kuandika majina yao.

Katika njia mbali mbali, msimamiaji wa mkutano anaweza kugawanya kikundi chote katika vikundi vidogo vidogo vya watu wanne au sita, na kuwapatia karatasi za kuandikia pamoja na markers peni, an kuwaomba na maoni yao ya kila kikundi. Katika hali hii vikundi vidogo vichaguliwe bila kufuata utaratibu wowote.Hasara moja wapo wa vikundi hivi ni baadhi wa washiriki watakuwa waoga au wakimya kuchangia mbele ya marafiki zao,au watu wanaofanya nao kazi kwa karibu, viongozi wao, au watu wanao wasimamia; Faida ya njia hii ni number ya washangaji imepunguzwa kwa sababu kujirudia rudia kwa mada, na watu wengine wanachangia zaidi katika kundi dogo kuliko wakiwa katika peke yao na karatasi.

Kuandika peke yako katika kipande cha karatasi, bila kuandika jina, inasaidia kuzuia mambo yasiotegemewa kwa mtoa mada, na kwa baadhi ya waangalizi mambo muhimu yanaweza kutolewa katika mikutano hii. Madhumuni ni kupunguza hali ya kutishwa kwa mshiriki na kumuakikishia mshiriki bila kuwa na woga, issue zote za Uimara,udhaifu,fursa na vikwazo zinaweza kuletwa tena kwa kukumbushia.

Kipindi cha SWOT ni kipindi shirikishi kwa maana kwamba washiriki wote wanapenda kuchangia katika matokeo ya mwisho. Ni sawa sawa na kipindi cha "Chemshabongo, ambacho kinategemea"Maswali manne muhimu ya Uongozi," lakini ni sawa zaidi katika groups kubwa katika kipindi cha kutauarisha Taasisi/organisation kwa kipindi cha mpito, au katika kipindi kinachopita kama vile kipindi cha nusu mwaka au mwaka mzima wa kupitia program.

The "Chemshabongo" ni njia nzuri kutumika katika kuanzisha mradi mpya au taasisi, inafanya kazi vizuri katika vikundi vidogo kuliko mikutano ya SWOT,na kinaweza kuwa kutumika vizuri katika hatua za mabadiliko, pale washiriki wanapokuwa katika vikundi vidogo vya viongozi.

Kusanya habari:

Kama habari imeandikwa katika karatasi nne, zinaitajika ziwekwe pamoja, mtu wa kujitolea au msaidzi wanaweza kukusanya katatasi zote, na kuweka pamoja katika mafungu manne, moja katika kila sehemu. Msimamizi,kwa kutumia ubao, aweke pamoja mawazo ya aina moja, na kuondoa zinazojirudia.

Kwa kufanya hivyo, msimamizi aonyeshe matokeo ni kazi ya kundi kwa pamoja, sio mawazo ya upande mmoja au kundi la moja.Hii ni muhimu, hasa pale kama kuna mabadiliko makubwa katika taasisi na maudhui wa program; wanachama wote wajisikie wapo sawa, ni kazi ya kila kundi na sio kazi ya kundi moja.

Kwa kufanya hivyo, msimamizi aonyeshe matokeo ni kazi ya kundi kwa pamoja, sio mawazo ya upande mmoja au kundi la moja.Hii ni muhimu, hasa pale kama kuna mabadiliko makubwa katika taasisi na maudhui wa program; wanachama wote wajisikie wapo sawa, ni kazi ya kila kundi na sio kazi ya kundi moja.

Kama vile katika kipindi cha chemshabongo, mwangalizi katika kila kundi, anaweza kwa kufuata umuhimu. Hii sio lazima kwenye mikutano ya SWOT, lakini itasaidia katika kuonyesha hali halisi ya matokeo yote.

Itakuwa vizuri kama msimamizi atafupisha maelezo,kwa kusaidiwa na washiriki, Mwangalizi mkuu wa kipindi mazoezi ya SWOT. Aonyeshe baadhi ya uimara kwa madhumuni hayo hayo inaweza ikawa udhaifu kwa madhumuni mengine, na analysis ya msimamizi yanaweza kuchangia katika malengo ya baadae ya taasisi.

Sawa na fursa kwa matendo fulani yanaweza kuwa vikwazo kwa malengo mengine.Pia ueleze matokea yatarekodiwa, na yatatumika kwa maandalizi ya kuandika malengo yanayoonyesha wapi organisation ipo na wapi inaenda?

Chunga maneno yako. usiache karatasi na manila sheets kupata vumbi katika shelf;Tumia information kuweka pamoja, kuandika kwa kifupi na kuanalysis, kwa kugawanya kwa washiriki. Hii inaweza kufanywa na kusambazwa ndani ya week moja baada ya mkutano.

Study inayotegemewa kuonekana

Study inakayotokana na washiriki isiusiche kitu kikubwa kisichotegemewa katika taasisi na wasimamizi wa program na muongozaji wa hiyo taasisi.

Uimara unausisha kuelewa kwa undani zaidi na uzoefu ulionekana na wafanyakazi. Baadhi ya uwelewa au utaalamu unaweza kutumika katika njia hiyo,lakin inaweza kuwa kikwazo cha kubadilisha program au taasisi.Kwa mfano,Program ya uwokoaji inaitaji kuwa na watu wenye uwelewa na uzoefu wa juu wa kuorodhesha, kusimamia na kupanga, na kufanya maamuzi, kwa kuangalia "demographic" na maesabu mengine, kwa niaba ya walioathiriwa na majangwa au mteja wa kikundi.Hii inaweza kuwa Uimara wa wafanyakazi wa kuibadilisha program pale ambapo maamuzi yanaitajika kufanyika na walengwa, na sio wasaidizi wa mawakala.

Kwa ujumla,kama wafanyakazi wana uwezo wa kusoma jinsi ya kufundisha wengine kwa uwezo waliokuwa nao, na wakajifunza jinsi ya kutoa, kusimamia na kazi za uunganishaji ya wakala, inaweza ikawa fursa zaidi kwa wakala kubadilisha program kutoka njia ya kutoa misaada, ni inaweza kuwa mzuri kuelekea kwenye taasisi nyingine ya kutoa misaada, au kuelekea sehemu nyingine ambapo taasisi itakuwa inafanya kazi, pale ambapo misaada ya dharura inaitajika.

Kama wafanyakazi wengi hawawezi kubadilisha program, maamuzi ya wakala inaweza kufunga kufanyakazi pale ambapo huduma ya haraka ya uokoaji haiitajiki, na kuruhusu program ya uwezeshaji kwa wakala mwingine kuja,na kuelekea nchi nyingine au mahali pengine ambapo Uimara wa taasisi unaitajika zaidi.

Maneneja, watu wa kupanga mipango,na wasimamizi wa wakala lazima wawe makini na matokeo ya mikutano ya SWOT katika kupanga maamuzi wapi pa kubadilisha, kufunga, kuendelea kama mwanzo, au kuelekea mahali pengine.

Itimisho:

Kipindi au Mikutano ya SWOT ni ya vikundi shirikishi ambavyo vinazalisha kitu kizuri kwa mipango ya kila mwaka au kwa kuamua mabadiliko makubwa ya program.

Ni nguvu inayotegemea vyanzo vya habari- wafanyakazi, watu waliojitolea, walengwa na au/ wadau wengine - wanajipanga kutoa mazingira yasioogopesha kwa kutoa nje hata vitu muhimu ambavyo havionekani katika mazingira mengine.

Set ya kuangalia kuhusu Uimara,udhaifu,fursa na vikwazo zinaweza kukusanywa na kupimwa, na kuondoa kujirudia rudia na kupanga "information" na kuwa mzuri kwa kuzalisha nakala ya kuangalia "hari ya baadae" ambayo itatoa muelekeo wa mafunzo kwa vitendo kwa taasisi (kwa wafanyakazi na watu wa kujitolea, washikadau, kupanga taasisi na program) ambayo inaweza kusaidia kusoma mabadiliko makuwa,au maono kwa kuangalia miaka ya mbele ya kujaribu na kukusanya mawazo ya ndani zaidi ya miaka iliyopita.

––»«––

SWOT Warsha / Semina


SWOT Warsha / Semina

© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
Web Design: Lourdes Sada
––»«––
Imeratibishwa mwisho: 08.11.2011

 Ukurasa wa nyumbani

 Janga