Ukurasa wa nyumbani
 Uhamashishaji




Fasiri:

Bahasa Indonesia
বাংলা / Baṅla
Català
中文 / Zhōngwén
English
Español
Filipino/Tagalog
Français
Galego
Ελληνικά / Elliniká
हिन्दी / Hindī
Italiano
日本語 / Nihongo
Kiswahili
Polszczyzna
Português
Română
Русский
Српски / Srpski
Tiếng Việt
اردو / Urdu

                                        

Kurasa nyingine:

Visomo

Ramani ya tovuti

Maneno muhimu

Wasiliana nasi

Nyaraka za matumizi

Tovuti zinazohusiana

KULA NA MARAFIKI

Umuhimu wa cha Chakula katika Kuwezesha Jamii

na Phil Bartle, PhD

imetafsiriwa na Wamalwa Philip


Kijitabu cha Mafunzo

"Nani anakula na nani" ni jambo ambalo linaadhiri uhamashishaji

Utangulizi:

Jambo moja muhimu la kuwezesha jamii ambalo mara nyingi hupuuzwa katika vitabu na mafundisho juu ya maendeleo ya jamii ni kula pamoja. Kwa mfano, sherehe ya kukamilisha mradi miongoni mwa shughuli nyingine muhimu, ambayo huweza kuchukuliwa na watu wengi kama likizo au "kuvuta pumzi", ni kati ya kazi muhimu ya mhamashishaji.

Kama vile mwana sayansi wa jamii atakuambia, kuna manufaa zaidi ya chakula kuliko tu hayo ya shibe na afya. Ni nani tunakula naye, lini, wapi, nini tunakula na katika mazingara gani... inamaana sana katika elimu ya jamii. (Ikiwa tunakula tu kwa sababu ya kushiba, basi sote tungekula minyoo au funza).

Kwa hivyo maswala haya ni muhimu sana kwa mhamashishaji, kwanza kwa kuijua jamii na jinsi mienendo yake itakavyokuwa katika jamii hiyo, na pili kwa kujumulisha maarifa hayo katika mipango ya kuimarisha jamii kupitia uhamashishaji.

Kula Pamoja:

Maneno haya "kula pamoja" inamaana sawa na neno "Commensal" ambalo ni neno la kiingereza lilitolewa kutoka kwa Kilatini (na Kiarabu), kumaanisha kushiriki meza moja. Katika sayanzi ya jamii, dhana hii ya "kula pamoja" imerahisishwa na kuwa "watu wanaokula pamoja."

Anza na wewe mwenyewe:fikiria ni watu gani ambao wewe hula nao na wale hauli nao. Kwa jumla, wale watu ambao wewe hula nao ni pamoja na familia yako na marafiki wako.

Wala ambao hauli nao, kwa sababu yoyote ile, ni wale ambao uko mbali nao katika uhusiano: wale wenye tabaka la juu au chini sana kuliko wewe, watu usiowajua, maadui na wapinzani wako wakuu, na mara nyingine watu kutoka kwa lugha iliyobaguliwa, kabila, dini, jinsia, umri au taaluma tofauti.

Bila shaka haya hubadilika badilika kutoka kwa jamii moja hadi nyingine na nyakati moja hadi nyingine. Pia hubadilika kulingana na mazingira ya kijamii; kuna watu ambao unaweza kula nayo katika mkahawa ulioko kazini, lakini huwezi kula nayo kwako au kwao.

Kwa jumla (isipokuwa kuna mambo ambayo yaweza kuwa tofauti), watu hupenda kula na wengine ikiwa tu kuna ile hali ya umoja au uaminifu. Wakati mwingine uaminifu huo waweza kufikiriwa tu kuwa upo hata ingawa huenda haupo; kwa mfano watu wengine hula na wengine ile kuonyesha uaminifu lakini hawaamini watu hao hata kidogo. Kula na wengine ni sawa na mambo mengine ya desturi na tamaduni, ni ishara, nayo inathibitisha maadili na maana nyingi.

Ushawishi ni Njia Mbili:

Uhusiano kati ya (a)hadhi ya jamii au urafiki na (b) nani anakula na nani, inajulikana na imethibitishwa. Hiyo haimaanishi kua kuwepo kwa moja ya hiyo kunasababisha lingine kuwepo, lakini inaonyesha kuwa uhusiano wa namna ile upo.

Ni namna gani moja inaweza kusababisha lingine? Wahamashishaji wenye uzoefu wanajua kuwa ushawishi wa mawili hayo ni njia mbili. Jinsi watu wanavyo fikiria kuhusu wengine inaweza kushawishiwa na ni nani anayechagua kula na nani. Vile vile, chaguo la ni nani anakula na nani yaweza kushawishiwa na jinsi watu wanavyo fikiria kuhusu wengine.

Hii ina maana mbili kwa mhamashishaji. (1) Jukumu la muhimu la mhamashishaji la kujua desturi na mila za jamii huweza kujulikana kwa kujua nani hula na nani. (2) Kuandaa chakula ambapo watu ambao kwa kawaida hawali pamoja wanapata kula pamoja ni njia moja bora ya kujenga uhusiano mpya wa kijamii na hivyo basi kukuza uwezo wa jamii kwa kuleta umoja.

Umoja ni jambo la maana sana kwa mhamashishaji.Tazama Kuleta Umoja. Ikiwa kuleta watu pamoja ili wale pamoja kutaboresha umoja wa jamii, basi hiyo inakuwa kifaa kingine katika kisanduku cha vifaa cha mhamashishaji.

Nafasi Tatu ambapo Chakula Kinaweza Kuandalia katika Uhamashishaji wa Jamii :

Kuna nafasi nyingi zinazoruhusu jamii au wanachama wa kamati kula pamoja hadharani. Jinsi mhamashishaji anavyofahamu jamii ndivyo atakavyotambua nafasi nyingi zaidi za kula pamoja.

Kwa kawaida, kuna nafasi angalau tatu:
  • Kuwapa chakula wafanyikazi wa jamii wakati wa ujenzi;
  • Kuandaa vinywaji katika mikutano ya kamati kuu; na
  • Kuandaa vinywaji katika sherehe.

Kuwapa chakula wafanyikazi wa jamii waliojitolea kufanya kazi kama ya kufagia na kusafisha kijiji au katika ujenzi wa mradi ni thamani kubwa sana ya kuongeza msisimko kazini na kujenga umoja na undugu.

Katika sehemu za mashambani, wakulima ambao hawana pesa za kutoa huenda waka changia kwa kutoa mazao yao.Wakati huo huo, wale watu ambao kwa sababu moja au nyingine hawawezi kufanya kazi nzito kama ya ujenzi wanaweza kutoa muda na nguvu zao kwa kupika na kuandaa chakula.

Ni rahisi kupuuza mchango wa kamati tekelezi au kamati kuu. Watu hao hutoa muda wao, ubunifu na maarifa yao kwa mradi wa jamii. Wanachama wa kamati hizo pia huwa makini kudumisha uazi jinsi wanavyotumia pesa na rasilimali ya jamii na hivyo basi kuimarisha imani na msisimko wa watu katika mradi huo. Ikiwa wanachama wa jamii wataandaa chakula kidogo na kuwapa wanakamati katika mikutano ya kamati, hata kama kwa kuonyesha ishara tu, basi haitakuwa rahisi kwao kushuku kamati hizi kuwa zina njama za kujitajirisha kwa kutumia vibaya mali ya jamii.

Katika sherehe za hadhara kukamilisha mradi, jamii huelezwa na mhamashishaji kuwaalika watu mashuhuri kuhudhuria na kusimamia. Hii huvutia wana habari ambao watatangaza sherehe hiyo. Ikiwa jamii itaonekana ikiwapa vinywaji wageni hao mashuhuri, na bora zaidi, kwa watu wote waliohudhuria, basi ujasiri na umoja wa jamii utaongezeka.

Kuchagua Chakula cha Kuliwa:

Mhamashishaji hapaswi kuchagua ni chakula gani kitaandaliwa. Kazi yake ni kuelekeza kamati au jamii iamue kwamba chakula kitaandaliwa, wakati upi, nini kitaandaliwa, wapi kitaandaliwa, kiasi kipi na kadhalika. Ikiwa kamati maalum ya kusimamia mambo ya chakula itaundwa, basi itakua chanzo kizuri cha habari kwa mhamashishaji.

Ikiwa chakula ambacho ni mwiko kitachaguliwa kama ndicho kitaandaliwa, basi hiyo itakuwa dalili ya mgawanyiko katika kamati kuu. Kwa mfano, nyama ya ngurue haipaswi kuandaliwa Waislamu, nyama yoyote haifai kupewa Wahindi au watu ambao hawali nyama. Ikiwa kamati itachagua moja kati ya chakula hiki ambacho hakifai, basi mhamashishaji atapata kidokezo kuwa kamati hiyo inapendelea upande mmoja wa vikundi vinavyozozana.

Mhamashishaji anapaswa kujaribu, kimya kimya kwa mara ya kwanza, kuishawishi kamati kuwa ni vyema izingatie tabia na mila tofauti ya ulaji katika jamii. Ikiwa hataweza kupata suluhisho kwa kufanya mambo kimya kimya, mhamashishaji anaweza kulizungumzia jambo hilo wazi wazi katika mkutano wa jamii nzima, akisisitiza kuwa mradi ni wa watu wote katika jamii, wala sio tu watu wa vikundi fulani na kwamba chakula kinachoandaliwa lazima kikubalike na wote au mpango ufanywe kutengeneza chakula maalum kwa ajili ya vikundi fulani.

Katika miradi mingi, hasa ikiwa wageni mashuhuri wanapewa vinywaji, imekuwa desturi kuandaa vinywaji maarufu vilivyo kwenye chupa (au mkebe). Mwandishi huyu haungi mkono kuandaliwa kwa vinywaji mashuhuri kama vya 'coca cola" na vingine. Maji yaliyochemshwa, vinywaji vinavyoandaliwa katika eneo hilo, chai au kahawa ni bora zaidi.

Muhtasari:

Desturi ya kula chakula pamoja, "wale wanaokaa meza moja," ni muhimu kwa mhamashishaji. Kujua tabia na jinsi watu wanavyokula ni kidokezo kizuri ikiwa mhamashishaji anaifahamu vyema jamii na huweza kutumiwa kujua iwapo jamii imeungana au imegawanyika.

Kuuliza jamii na kamati kuu ya mradi kuweka wakati ambapo watu wanaweza kula pamoja, itakuza umoja, undugu na imani, ambavyo ni viungo muhimu vya kuwezesha jamii.

Jinsi tu ambavyo mhamashishaji mzuri anavyofanya mambo mengine, vile vile katika mambo ya chakula, mhamashishaji atatumia mbinu ya kushirikisha jamii, akiielekeza na kusisimua jamii na kamati kuu yake kufanya maamuzi, badala ya kuamuru na kufanya maamuzi mwenyewe.

Marejeleo:

Chakula na Utamaduni: http://lilt.ilstu.edu/rtdirks/SOCIAL.html

Margaret Visser: http://www.umanitoba.ca

––»«––

Mchango wa Jamii: Chakula Kilichotolewa kwa Wafanyakazi wa Kujitolea:


Mchoro14
 Nyumbani

 Uhamashishaji