Ukurasa wa nyumbani
 Uhamashishaji
Fasiri:

বাংলা / Baṅla
Català
中文 / Zhōngwén
English
Español
Filipino/Tagalog
Français
Galego
Ελληνικά / Elliniká
हिन्दी / hindī
Italiano
日本語 / Nihongo
Kiswahili
Polszczyzna
Português
Română
Русский
Српски / Srpski
Tiếng Việt
اردو / Urdu

                                        

Kurasa nyingine:

Visomo

Ramani ya tovuti

Maneno muhimu

Wasiliana nasi

Nyaraka za matumizi

Tovuti zinazohusiana

KULETA UMOJA

na Phil Bartle, PhD

imetafsiriwa na Wamalwa Philip


Kijitabu cha Mafunzo

Ijapokuwa "kuleta umoja" mara nyingine huitwa hatua ya tatu katika kipindi cha uhamashishaji, kuleta umoja inaweza kuanza hata katika hatua ya kwanza (ya kufahamisha) na kuendelea katika kipindi chote cha uhamashishaji.

Si Rahisi kupata Jamii ikiwa Imeungana:

Neno "jamii" linaashiria kuwepo kwa umoja, lakini ni makosa ya kawaida watu kufikiria kuwa jamii yoyote huwa na umoja.

Kila jamii ina vikundi na ugomvi ndani yake ambayo tunaita migawanyiko ya kijamii.Hii huweza kusababishwa na dini, ukoo, tabaka, lugha, tofauti za kikabila na mambo mengine.

Ufafanuzi: A "mgawanyiko" ni utengano au shimo kubwa kati ya pande mbili tofauti. "Mgawanyiko wa kijamii" ni utengano kati ya vikundi viwili au zaidi katika jamii kubwa.

Maamuzi ya Jamii Yanahitaji Umoja:

Ikiwa tunataka jamii kufanya uamuzi kwa masikizano ili kukubaliana juu ya shida ambazo zitapewa kipao mbele katika utatuzi, hiyo haiwezekani ikiwa vikundi tofauti vinaunga mkono malengo tofauti.

Kwa hivyo kuleta vikundi hivi pamoja na kuendeleza umoja, ni kazi muhimu yako wewe, mhamashishaji. Je utafanyaje hayo?

Mbinu ya Kuunganisha Jamii:

Wakati unapoitisha mkutano, hakikisha kuwa vikundi vyote tofauti vimehudhuria. Hakikisha pia kuwa mkutano huo unajumulisha watu wenye ulemavu, wakongwe na wale husahauliwa mara kwa mara.

Iwapo umefanya kazi yako vyema katika elimu ya jamii, ukiichunguza na kuidadisi, basi utajua ni wapi ambapo maswala nyeti yapo.

Ni muhimu kuwa muigizaji au "mwana sarakasi" kidogo wakati unapohamashisha. Kwa mfano unaweza kutumia mifano ya vijiti vya kiberiti, lakini chukua muda wako. Ita mtu au watu wawili wa kujitolea wakusaidie, rudia wewe mwenyewe peke yako kwa njiia tofauti; fanya iwe kama sarakasi. Inua juu kijiti kimoja cha kiberiti na uulize kikundi kikweleze ikiwa itakuwa rahisi kukivunja.

Pata maoni yao. Kisha uliza yule mtu aliyejitolea akivunje. Mpongeze sana yule mtu wa kujitolea na ufanye mzaa na kikundi hicho jinsi ilivyokua rahisi kukivunja kijiti hicho.Halafu sasa uchukue vijiti vilivyojaa mkononi na uvifunge pamoja kwa kamba; onyesha kikundi kibunda hicho cha vijiti. Haya, sasa tena muulize yule mtu wako wa kujitolea avunje kibunda hicho cha vijiti kama kitu kimoja. Mtu yule atakuwa na ugumu au (tunatumaini) hataweza kuvunja kibunda hicho cha vijiti vya kiberiti.

Hapo utasema kuwa kila kijiti kunaashiria kikundi tofauti na kibunda cha vijiti ni jamii kwa jumla ikiwa imeungana. Umaskini na udhaifu vinaweza kuivunja jamii kwa urahisi ikiwa vikundi hivyo vitaendelea kujitenga.

Onyesha kikundi vijiti hivyo tena wakati unapoelezea ulinganivu huo (au simile au fumbo) huku ikionyesha kijiti kimoja wakati unapotambua kikundi na ujaribu tena kuvunja kibunda cha vijiti wakati unapokilinganisha na jamii ilio na umoja. Fanya hivi mara kadhaa katika mikutano katika wakati tofauti. (Usiogope wala kuchoka kurudia rudia kanuni muhimu).Endeleza ujumbe huu kwa mifano na hadithi ambazo umetunga mwenyewe au kupata kutoka kwa wahamashishaji wengine.

Tazama: Jukumu la Chakula katika Kuwezesha Jamii.

Tazama: Kuimarisha Jamii.

Lengo lako sio kufanya kila mtu katika jamii kuwa wa tabia sawa lakini ni kuwawezesha watu wawe ni wenye kuelewa na kuvumilia tofauti zao na wengine kwenye jamii na wawe waaminifu na kuunga mkono jamii yote.

Usiwache:

Unganisha huu mfano na juhudi tofauti za kuleta umoja, kwa mfano kwa kuhakikisha kuwa kila kikundi kinapata nafasi katika kamati kuu ya shirika ambalo utaunda kutekeleza mradi huo.

Umuhimu wa kuleta na kudumisha umoja unaendelea katika mradi mzima na juhudi za kuleta umoja hazipaswi kuachwa wakati unapokwenda kwenye hatua nyingine. Kutana na wahamashishaji wengine na kuwafunza na kujifunza mbinu mipya.

––»«––

© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
Web Design: Lourdes Sada
––»«––
Imeratibishwa mwisho: 11.11.2011

 Nyumbani

 Uhamashishaji