Ukurasa wa nyumbani
 Kuudhibiti Muingiliano




Tafsiri:

'العربية / al-ʿarabīyah
Bahasa Indonesia
বাংলা / Baṅla
Български език
Català
中文 / Zhōngwén
Deutsch
English
Español
Filipino/Tagalog
Français
Galego
Ελληνικά / Elliniká
हिन्दी / hindī
Italiano
日本語 / Nihongo
Kiswahili
Português
Română
Русский
Српски / Srpski
ไทย / Thai
Tiếng Việt
Türkçe
اردو / Urdu

                                        

Kurasa nyingine:

Visomo

Ramani ya tovuti

Maneno muhimu

Wasiliana nasi

Nyaraka za matumizi

Tovuti zinazohusiana

UONGOZI WA JAMII NA UCHOCHEZI WA NDANI

Kudhibiti kwa Uchochezi wa hiari

na Phil Bartle, PhD

Imetafsiriwa na Lillian Odembo Naka


Kifafanuzi cha mafunzo

Muingilio wako kama mchochezi au muhudumu wa jamii ulikuwa wa kutoka nje ya jamii hiyo; ili kudhibiti maendeleo,jamii yenyewe inafaa kuendeleza huo muingiliano.

Jambo muhimu katika kudhibiti muingilio wa kuisisimua jamii kujiongezea uwezo wa kujitegemea, upo ndani ya jamii yenyewe. Shirika lako laweza kupenda au kuwa na uwezo wa kukupa mrithi, lakini lengo lako kubwa ni kuiacha jamii iendelee kujichochea.

Utakavyo fanya ni kutafuta watu kutoka kwa jamii hiyo, walio na uwezo wa kuchochea jamii na pia wana nia na maadili mema, kisha uwafunze ujuzi wako ili wakurithi baadaye.

Nia yako ni kujitoa.

Ustawishaji wa jamii ni harakati ya kuleta mabadiliko katika jamii hiyo. Sio wewe unayeistawisha jamii bali ni jamii yenyewe inayojistawisha.

Waweza kuwa changamoto katika harakati hiyo.Dondoo kutoka kwa mwalimu Julius Nyerere, "Watu hawawezi kuendelezwa; wanaweza kujiendeleza wenyewe binafsi".

Kumbuka pia kwamba vifaa na ujuzi ulionao,vyaweza kutumika kwenye harakati hiyo ya kuleta mabadiliko. Kifaa chochote chaweza kutumiwa vibaya.Utakapo watambua wenyeji watakao kurithi, ni muhimu kuchunguza tabia zao na kuhakikisha kwamba watavitumia vifaa vya uchochezi kwa manufaa ya jamii na wala sio kwa manufaa yao wenyewe.

Ni vyema kutambua kuwa watu wengine wana lengo au malengo ya kisiasa.Mtu aliye na ujuzi mzuri wa ushirikishi na usahilishi, aweza kutumia shughuli ya uchochezi kwa manufaa yake mwenyewe. Tazama tena Tambua Ujuzi Unaohitaji na tamthili ya "fundi wa kufuli na funguo".Utakapo watambua watu wenye uwezo wa uchochezi,unapaswa kuwapeleleza kwa muda. Usiwe na haraka ya kupata mrithi; chukua wakati ili ufaulu.

Unapo elezea kundi fulani juu ya kuchukua muda ili kufanya kitu inavyostahili, waweza kuwaelezea hadithi ya fahali wawili kutoka kwa jamii ya wafugaji ng'ombe huko Africa Magharibi.

Fahali wawili walikua wakishuka toka juu mlimani, wakawaona zaidi ya Ng'ombe mia moja chini ya mlima huo. "Oh, Mjomba,"akasema fahali mdogo,"Tukimbie chini tukawafanye ng'ombe wachache". "La",akajibu fahali mkubwa, "Tutembee hadi chini na tuwafanye ng'ombe wote".

Chukua muda wa kutosha ili kumsaka na kumfunza mrithi wako.

Utakapo pata watu wenye uwezo wa kuwa wachochezi wa jamii, wenye maadili kama, uaminifu,uongozi mwema,wenye nia ya kuleta maendeleo kwa jamii; unahitajika kuwafunza. Wakipenda, unaweza kuwaweka kama "wanafunzi", na uchukue muda kuwaelezea sababu ya kitendo au vitendo vyako.

Hakikisha umefanikisha au kupitia mashauri yote kwenye sura chache za mwanzo.Kuwasaidia kujifunza kanuni za msingi ni muhimu sawa na wao kujifunza ujuzi walionao. Wape nafasi ya kuongoza vikao vya usahalishi au mafunzo mara kwa mara ili kukuza ujuzi wao. Watakapo kamilisha mizunguko miwili au zaidi ya uchochezi wa jamii, wanastahili kuwa tayari kuendelea bila uwepo wako.

Unaelekea kulifanya jukumu lako la uchochezi wa jamii kudhibitiwa.

––»«––

© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
Web Design: Lourdes Sada
––»«––
Imeratibishwa mwisho: 12.11.2011

 nyumbani Ukurasa

 Kudhibiti muingiliano