Ukurasa wa Nyumbani
Matayarisho
Tafsiri:

বাংলা / Baṅla
Bahasa Indonesia
Български език
Català
Cebuano / Sugboanon
中文 / Zhōngwén
Deutsch
English
Español
Euskara
Ewe
Filipino/Tagalog
Français
Galego
Ελληνικά / Elliniká
ગુજરાતી / Gujarātī
हिन्दी / hindī
Italiano
日本語 / Nihongo
Kiswahili
بهاس ملايو / Bahasa Melayu
Polszczyzna
Português
ਪੰਜਾਬੀ / Pañjābī
Română
Русский
सिन्धी / Sindhi
Af Soomaali
తెలుగు /Telugu
ไทย / Thai
Tiếng Việt
Türkçe
اردو / Urdu
Èdè Yorùbá

                                        

Kurasa nyingine:

Visomo

Ramani ya tovuti

Maneno muhimu

Wasiliana nasi

Nyaraka za matumizi

Tovuti zinazohusiana

TAMBUA MAARIFA UNAYOHITAJI

Unahitaji Nini, Kujua Jinsi gani ya Kufanya?

na Phil Bartle, PhD

Imetafsiriwa na Elie Chansa


Kitini cha Mafunzo

Maarifa unayohitaji kwa ajili ya kuratibu

Maarifa unayohitaji kama mratibu, kimsingi siyo marahisi kujifunza, lakini yanaweza kuwa vitendea kazi muhimu sana. Lakini pia yanaweza kutumika isivyopaswa.

Kama mlinganishaji, hebu fikiria ujuzi alionao fundi vitasa. Ujuzi huo unatumika kwa manufaa na huduma muhimu nyingi tu, ila unaweza pia kutumika kuvunja, kuingia, na kuiba.

Utapokuwa unajifunza ujuzi wa kuratibu, utumie kwa manufaa ya jamii, siyo kujinufaisha mwenyewe kwa gharama ya jamii.

Kwa kuwa kundi lengwa ni jamii kwa ujumla, maarifa mengi unayohitaji yapo kwenye uwezo wa mawasiliano. Unahitaji kujifunza kuwa mzungumzaji kwenye umma, ila siyo kama mzungumzaji yeyote wa umma. Uzungumzaji wa umma unaohitaji ni ule unaotakiwa kwa ajili ya uongozi na uwezeshaji.

Yakupasa kujifunza jinsi ya kupata taarifa na kufanya maamuzi toka kwenye kundi, kitu ambacho kinahitaji uelewa mkubwa wa malengo yako na kujiamini mbele za watu.

Yakupasa uwe mtambuzi wa mahubiri, mihadhara, na kuhutubu, na ukwepe aina hizo.

Mbinu za kiufundi unazohitaji kama mratibu zinahusisha: uzungumzaji kwenye umma, mipango, kuongoza, kuchunguza, kuchambua, na kuandika. Njia bora ya kujifunza haya ni kupitia kujifunza mwenyewe.

Inabidi pia ujijengee tabia ya uaminifu, kuridhika, kuwa mwenye mawazo chanya, kukubaliana na wengine, uvumilivu na hamasa.

Inakubidi ujue kusikiliza na kuelewa watu wanapoongea.

Inakubidi ujue jinsi ya kuhakiki taarifa kuwa ni sahihi.

Inakubidi ujue jinsi ya kueleza mada na kuifanya iwe ya kuvutia kwa msikilizaji.

Hutakiwi; kuhubiri kama mchungaji, kuhutubia kama mwanasiasa, kuhadhiri kama profesa.

Unatakiwa kujifunza jinsi ya kuwa mwenye kujiamini na kuwa makini kwa wengine unapokuwa miongoni, ama mbele ya watu wengi.

Unatakiwa kujua jinsi ya kujua na kupenda watu.

Unatakiwa kujua jinsi ya kujizuia kutingwa na mambo binafsi, mambo yasiyo na msingi, au majigambo.

Unatakiwa kujua kuongoza mjadala bila kujikweza, kuongoza kidikteta ama kukejeli.

Jifundishe haya mwenyewe

Unajifunza ujuzi huu kwa kutenda (sio kwa kusoma kitabu tu).

Kama ulienda kwenye darasa la maendeleo ya jumuiya, na ukaishia kukaa na kuandika kumbukumbu, hukupata mafunzo bora. Inakupasa ufanye kwa vitendo. Kwanza, mbele ya darasa lako, kisha mbele ya kundi la wanajumuiya. Tazama Mbinu za Mafunzo

Kwa kuwa unatakiwa kuratibu makundi ya wanajumuiya na kuunda kamati za utendaji unahitaji baadhi ya mbinu za kuratibu ujuzi..

Kwa kuwa pia unakomaa kwa kutoa ujuzi wa uongozi, unahitaji pia ujuzi wa uongozi mwenyewe.

Kwa kuwa unaongoza vikundi vya wanajumuiya kwenye mipango yao wenyewe, unahitaji pia ujuzi wa mipango mwenyewe.

Kwa kuwa unashauri na kuongoza makundi kuhifadhi kumbukumbu za mahesabu kwa uhakiki na uaminifu, unahitaji pia ujuzi wa mahesabu mwenyewe

Kwa kuwa unaongoza makundi kuandika ripoti na unahitaji kuandika ripoti zako mwenyewe, unahitaji ujuzi wa kuandika.

Jifunze kwa kutenda.

Unahitaji kujua kujifunza lugha haraka, (tazama Mbinu ya kusikia na kujifunza lugha ya mazungumzo) na kuwa na upeo kuhusu lugha mbalimbali kwenye jumuiya.

Zaidi ya ujuzi wa kiufundi, unahitaji kuwa na tabia binafsi ambazo zinafaa kukuwezesha kuwa mratibu. (Angalia kitini cha mafunzo: Kuwa Mratibu na Maelezo ya Kazi).

Sifa yako ndio amali yako kuu. Kama unajulikana kwa kuwa mwaminifu, mwenye kujali, kiasi, bidii, maadili, maisha mema, kukubaliana na wengine, kuridhika, unyenyekevu, na uwazi, sifa zako zitarahisisha juhudi zako za uratibu. Kama huna hizo sifa, tafuta wito mwingine, ama kazi ambayo una mzigo nayo.

––»«––

© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
Web Design: Lourdes Sada
––»«––
Imeratibishwa mwisho: 12.11.2011

 Ukurasa wa nyumbani

 Matayarisho