Ukurasa wa Nyumbani
Matayarisho
Tafsiri:

'العربية / al-ʿarabīyah
বাংলা / Baṅla
Bahasa Indonesia
Български език
Català
Cebuano / Sugboanon
中文 / Zhōngwén
Deutsch
English
Español
Euskara
فارسی / Fārsī
Filipino/Tagalog
Français
Galego
Ελληνικά / Elliniká
हिन्दी / hindī
Italiano
日本語 / Nihongo
Kiswahili
بهاس ملايو / Bahasa Melayu
Português
ਪੰਜਾਬੀ / Pañjābī
Română
Русский
Af Soomaali
తెలుగు /Telugu
ไทย / Thai
Tiếng Việt
Türkçe
اردو / Urdu
Èdè Yorùbá

                                        

Kurasa nyingine:

Visomo

Ramani ya tovuti

Maneno muhimu

Wasiliana nasi

Nyaraka za matumizi

Tovuti zinazohusiana

RASILIMALI ZA NJE

Kuweka Uwiano kati ya Rasilimali za Ndani na Nje

na Phil Bartle, PhD

Imetafsiriwa na Elie Chansa


Kitini cha Mafunzo

Msaada kiasi gani unaweza kuja kutoka nje ya jumuiya kabla jumuiya  haijawa tegemezi kwa msaada wa nje, na hivyo kupoteza uwajibikaji binafsi?

Kama mratibu, utaona kuwa ni vigumu kuwa na uwiano kati ya rasilimali zitokazo nje ya jumuiya, na zile za ndani.

Wewe na viongozi wa jumuiya mtakuwa katika presha kubwa tu, ili kuleta rasilimali za nje kwenye jumuiya.

Mashirika wafadhili wanataka kusaidia wakati wanajumuiya wanataka kupokea.

Unafamu hata hivyo, kuleta rasilimali za nje kunachangia gonjwa la utegemezi na kupunguza uwezo wa ustahimilivu na kujitegemea.

Licha ya hivyo, kuna njia za kuongeza uwezo wa kutumia rasilimali za nje, kama ilivyooneshwa kwenye hadithi ya Mohammed na kamba. (Tazama Kuhadithia).

Kama unaweza kushawishi wafadhili wa nje kugharamia mafunzo ya maarifa, mafunzo ya uongozi, na uratibu, na kuwezesha jumuiya kupata rasilimali ujenzi kadhaa za kwao, utaweza kuchangia kwenye kujitegemea na ustahimilivu.

Kama Mtume, amani iwe juu yake, angempa chakula ombaomba, angekuwa anamfudisha ombaomba kuwa ombaomba; kwa kumpa ushauri na mtaji badala yake, alimsaidia ombaomba kuwa mwenye kujitegemea.

Mtandao huu unakusaidia kupata rasilimali za nje, kama kwenye Michanganuo, itakayokusaidia kuandaa michanganuo yenye nguvu.

Kama chombo chochote chenye nguvu (kwa mfano, moto), maarifa haya yanaweza yasitumiwe ipasavyo na yanaweza kuchangia kwenye umaskini kwa mtazamo wa muda mrefu.

Yatumie vizuri, kwa ajili ya mwisho sahihi.

──»«──

© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle
Web Design: Lourdes Sada
––»«––
Imeratibishwa mwisho: 12.11.2011

 Ukurasa wa nyumbani

 Matayarisho